Sunday, June 17, 2012

Tofauti kati ya Biblia na Kitabu cha Neno la Mungu

Kulingana na matumizi ya Lugha, neno biblia linatokana na neno la Kiyunani (Greek) lenya mizizi yake katika mji wa kale wa bandari katika pwani ya nchi ya Finike (Phoenicia) ulojulikana kama Byblos. Jina hili lilitokana na biashara ya kutengeza bidhaa kama makaratasi yaliyotumiwa kuandikiwa vitabu. Makaratasi haya yalitengezwa kutokana na minyaa (reeds)ijulikanayo kwa Kiingereza kama papyrus au byblos , Hivyo basi neno hili likachukua maana hii na kufikia karne ya pili baada ya Kristo(AD), Wakristo wakiyunani waliyaita Maandiko matakatifu  ta Biblia (τα βιβλία) lenye maana vitabu.

Neno hili likaendelezwa katika lugha ya Kilatini na kiambishi asilia( prefix) 'ta' kikadondolewa. Neno hili likaenedelezwa tena katika Kifaransa na wingi wake wa biblos "VITABU" ukapuuzwa na UMOJA wake Le Bible ukapitishwa vivyo hivyo katika Kiingereza kama tulijuavyo sasa-BIBLE.

Biblia imetafsiriwa katika lugha nyingi kwa mfano huko Kenya katika  lugha ya Kikuyu biblia inajulikana kama Ibuku ria Ngai (kitabu cha Mungu) katika Kijaluo, Muma Maler katika Kimaragoli inajulikana kama Kitabu Kitakatifu na katika Kiwanga, lahaja mojawapo ya Kiluhya biblia inajulikna kama Ibublia.

Kwahivyo kulijibu swali lililozua mada hii, kitabu hicho ulichokiona kiitwacho Kitabu cha Neno la Mungu ni mojawapo ya tafsiri nyingi za Biblia amabzo zinajaribu kurahisisha lugha iliyotumiwa katika kutafsiri nakala au toleo za awali. Lakini neno biblia lina maana ya maktaba kwani Biblia ni mkusanyiko wa vitabu kadhaa.(66) Fauka ya hayo, tahadhari ni sharti ichukuliwe kwa sababu tafsiri nyingi zimebadilisha maana linge iliyodhamiriwa na waandishi wa asilia. Shukrani.

No comments:

Post a Comment